Gari Aina ya Pro Box Ikiwa 
tayari kusafirisha abiria
 Wakazi wa Mkoa wa Geita maeneo ya Buseresere na Katoro wapo katika hatari kubwa ya maisha yao kutokana na usafiri wanaoutumia kutoka eneo moja kwenda jingine.
Mwakilishi wa kikundi cha usalama barabarani Fungo Agustus ametutumia Tukio hili ambalo ni hatari kwa abiria mkoani Geita.
Gari ndogo aina ya Pro Box zimeingia kwa wingi mkoani Geita na kutumika kubebea abiria katika mazingira ambayo si salama na ni hatarishi kwa abiria hao.
Abiria wamekuwa wakipakiwa kwenye mabuti ya kuwekea mizigo tena kwa msongamano mkubwa.Zifutazo chini ni picha za kinachoendelea kwenye usafirishaji eneo la Buseresere.                         

 Abiria wakiwa wamekusanywa kwenye buti eneo la kubebea mizigo huku wakiwa sambaba na watoto wadogo.
 Aina nyingine ya Gari ndogo inayotumika kubebea abiria
 Mizigo na Watoto wakiwa wamekusanywa pamoja na mizigo nyuma ya Gari hiyo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 30, 2015

    Gari zimejaa hapa Dar-es-Salaam mpaka zinasonngamana kwenye foleni si wangezipeleka mikoani watu waache kujazwa kama mizigo.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 01, 2015

    Boda boda zilizojaa hivyo Dar na nyingine wangesogeza huko wakapata biashara nzuri tuu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...