Kampuni na taasisi zinazotoa huduma katika bandari ya Dar es Salaam zimeshauriwa kuanza kufikiria kuhamia katika jengo jipya la kisasa la Mamlaka ya Bandari Tanzania (kushoto) kama moja ya kuimarisha huduma za bandari. 
Akizungumza na timu ya wahariri waliotembelea bandari hiyo hivi karibuni, Kaimu Meneja wa bandari ya Dar es Salaam, Bw. Hebel Mhanga alisema mbali na kuwa makao makuu ya TPA, jengo hilo litakapokamilika litakuwa na kampuni na taasisi mbalimbali zinazohudumia bandari. 
“Hiki kitakuwa ni kituo kimoja cha kutolea huduma za bandari...tunakaribisha maombi ya nafasi toka kwa wadau wetu mbalimbali,” alisema. 
Jengo hilo la ghorofa 35 litakuwa kati ya majengo marefu kabisa jijini. Tayari baadhi ya taasisi kama Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Ofisi ya Mkemia Mkuu na wakala wa Mizani na Vipimo tayari zina madawati yao TPA. 
Meneja huyo alisema kuwa kama kampuni na taasisi nyingine zitafanya hivyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha huduma za bandari na kuifanya kuwa shindani. “Ujenzi wa jengo hili ni moja ya hatua za serikali kuimarisha huduma za bandari hii,” alisema. 
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Kimataifa cha Makasha (TICTS), Bw. Paul Wallace alisema wanazidi kununua vifaa vya kunyanyulia mizigo vya kisasa zaidi kuhudumia shehena ya mizigo inayozidi kuongezeka siku hadi siku. 
“Tumejipanga kuhudumia kwa wakati na ufanisi na hivyo kuchangia kuimarisha bandari hii,” alifafanua. 
Alisema bandari hiyo inahitaji kuwa na kina kirefu ili kuwezesha meli kubwa zaidi kutia nanga na pia kuwa na mtandao mzuri wa barabara na reli unaounganisha Tanzania na nchi jirani. 
“Majukumu haya ni ya serikali na wadau wengine kwa ujumla,” alieleza. Alisema TICTS inaendelea kuimarisha huduma zake ili kuifanya bandari kuwa kimbilio katika eneo hili la Africa. 
“Bandari inaimarika kwa haraka...kuna kila sababu ya sisi kuwekeza zaidi hapa,” aliongeza.
 Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Hebel Mhanga (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Kitengo cha Kimataifa cha Makasha (TICTS), Bw. Paul Wallace wakati wa ziara ya wahariri wa vyombo vya habari katika bandari ya Dar es Salaam hivi karibuni.  Wahariri hao walitembelea maeneo mbalimbali katika bandari hiyo.
Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Hebel Mhanga (kulia) akiwaelezea jambo wahariri wa vyombo vya habari katika bandari ya Dar es Salaam hivi karibuni.  Wahariri hao walitembelea maeneo mbalimbali katika bandari hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Ndio tunavohitaji nasi hapa kwetu tanzania tuwe na Marengo marefu hadi kufikia ghorofa 100-150
    Iwe mfano kwa nchi za africa verynice

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 21, 2015

    Mbona jengo halijanyooka? Limepinda!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 22, 2015

    Tuwekeeni video ya jengo hilo la TPA ili kuweza kupata wapangaji wa kutoka kila sehemu ya dunia badala ya kuweka picha mgando pekee yake. Video iwe ya ubora wa HD na paramonic view ya maeneo degree 360.

    Youtube ipo bureeee! bila malipo changamkeni! kwa ajili pia ya kufahamisha potential customers wa bandari na majengo yake.

    Mdau
    Christos Papachristou
    Diaspora.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...