Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Idara ya Oganezesheni Dr Mohamed Seif Khatibu akizungumza na Waandishi wa Habari makao makuu Dodoma kuhushu ratiba ya kuchukua fomu leo  Wagombea Urais kupitia Chama hicho aliwataja kuwa ataanza Prof Mark  Mwandosya ,Stephen Wasira,Edward Lowasa, balozi Amina Salumu Ali na Charles Makongoro Nyerere  na Khatibu ndiye aliyepewa jukumu na Chama hicho kutoa fomu hizo.

Wanasiasa watano  wanatarajia kuchukua fomu ya kugombea urais  katika makao makuu ya chama cha Mapinduzi (CCM) Dodoma.

Kwa mujibu wa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) wa Oganaizesheni, Dk Muhammed Seif Khatib, uchukuaji wa fomu hizo unaanza rasmi leo.

Amesema kwa mujibu wa orodha waliyonayo, wanachama watano watachukua fomu hizo kuanzia saa nne asubuhi hadi saa 10:30 jioni, na kila mmoja amepewa saa moja na wametenga muda wa kuzungumza na waandishi wa habari kwa wagombea ambao wataona inafaa kwao. Amemtaja wa kwanza kuchukua fomu kuwa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu), Profesa Mark Mwandosya kuanzia saa 4 kamili hadi saa 5:30.

Profesa Mwandosya atafuatiwa na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Stephen Wassira kuanzia saa 5:30 na atafuata Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa atachukua fomu kuanzia saa saba kamili. Wa nne atakuwa Waziri wa zamani wa Muungano, Balozi Amina Salum Ali kuanzia saa 8:30 mchana na pazia la ufunguzi litafungwa saa 9:30 alasiri na mtoto wa Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, Charles Makongoro Nyerere.

Baada ya kumaliza kuchukua fomu  kwa kundi la kwanza wanasiasa  wengine ambao wametangaza nia ya kuwania urais ni Lazaro Nyalandu, Frederick Sumaye, Profesa Sospeter Muhongo, January Makamba, Mwigulu Nchemba na Luhaga Mpina.Wanaotajwa ni pamoja Bernard Membe, William Ngeleja, Dk Titus Kamani, Luhaga Mpina, Mizengo Pinda, Dk Asha-Rose Migiro, Shamsi Vuai Nahodha, Dk Emmanuel Nchimbi na Dk Hamis Kigwangalla.

Katibu huyo wa Oganaizesheni amesema uchukuaji huo wa fomu utazingatia taratibu zilizowekwa na CCM na kutakuwa na fomu tatu zitakazopewa wagombea.Fomu  ya kwanza  itahusu maelezo binafsi ya mgombea, itahusu uzoefu na ujuzi wake, nyingine itakuwa ya kujaza orodha ya wadhamini wake na nyingine ya masharti kama yalivyokubaliwa na Halmashauri Kuu ya Taifa.

Kwa upande wa wadhamini  amesema, mgombea atatakiwa kupata wadhamini 450 kutoka katika mikoa 15 ya Tanzania Bara na mikoa mingine mitatu ya Tanzania Zanzibar. wagombea hao watakapofika kuchukua fomu, wanapaswa kuwa na ada ya Sh milioni moja na watasaini daftari maalumu kuonesha ndio waliochukua fomu.

Amewataka  wagombea wengine wanaotaka kuchukua fomu hizo kuwasiliana mapema na ofisi yao kwani alisema wangependa kazi ya uchukuaji fomu kudumu kwa siku zisizozidi tano ili shughuli nyingine ziendelee.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...