Mwenyekiti wa UWT Mufindi na mjumbe wa NEC Taifa Bi Marcelina Mkini akiwapongeza wanawake kwa kuonyesha kumkubali
Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Mufindi Bi Marcelina Mkini wa kwanza kushoto akiwa na mkuu wa wilaya ya Mufindi Mboni Mhita na mwenyekiti wa UWT mkoa wa Iringa Bi Zainabu Mwamwindi wakati wa kongamano la wanawake wilayani Mufindi.
WAKATI joto la uchaguzi mkuu likiendelea kushika kasi ndani ya chama cha mapinduzi (CCM) kwa wanachama wake kujitokeza kutia nia ya kuwania urais ,ubunge na udiwani , umoja wa wanawake Tanzania (UWT) wilaya ya Mufindi umemuomba mwenyekiti wa UWT wilaya ya Mufindi Marcelina Mkini kugombea nafasi ya ubunge jimbo la Mufindi kusini .
Wakizungumza mara baada ya kumalizika kwa kongamano la UWT wilaya ya Mufindi wajumbe wa kongamano hilo walisema kuwa toka nchi ipate uhuru wake mwaka 1961 wilaya ya Mufindi mkoani Iringa haijapata kuwa na mbunge mwanamke hivyo kwa uchaguzi wa mwaka huu lazima wanawake wachukue nafasi ya kuongoza ubunge jimbo la Mufindi kusini ambalo kwa sasa linaongozwa na mbunge Mendrady Kigola (CCM).
Haya safari hii ni zamu ya wabunge KUOMBWA.
ReplyDeleteKina mama mkijisikia mnaweza muhamasiki kuchukua fomu msingoje tu viti maalumu hata nyinyi mnatosha na kuweza kuongoza.
ReplyDelete