Mwenyekiti wa Baraza la wadhamini la Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania, Shehe Abdallah Ndanga (kushoto), akizungumza wakati wa kongamano kuhusu ‘Msimamo Mkali katika Dini, Maana, Matukio, Sababu na Suluhisho’ lililowashirikisha viongozi kutoka zaidi ya misikiti 100 , viongozi wa taasisi za kiislamu, wanazuoni, na vijana wanaoendesha harakati za kiislamu katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wengine kushoto kwake ni baadhi wa viongozi wa umoja huo; Shehe Suleiman Amrani Kilemile, Shehe Muharram Juma Doga na Shehe Ibrahim Hamadi.
Baadhi ya washiriki wa kongamano la siku moja lililokuwa likijadili kuhusu ‘Msimamo Mkali katika Didi, Maana, Matukio, Sababu na Suluhisho’ lililoandaliwa na Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania na kufanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mmoja wa washiriki wa kongamano hilo akitoa mchango wake wa mawazo kuhusu mjadaala uliokuwa ukiendelea.
Baadhi ya washiriki wa kongamano hilo wakipiga picha ya kumbukumbu. Ilielezwa kuwa suala la msimamo mkali katika dini linapingana na imani na mafundisho sahihi ya uislamu likichangiwa pia na ukosefu wa elimu sahihi ya dini ya kiislamu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...