Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya kuratibu Harambee ya kuwachangia waandishi wa habari wanaougua maradhi mbalimbali ikiwemo ugonjwa sugu wa saratani Bw. Benjamin Thompson Kasenyenda akitoa wito kwa watanzania wote wenye mapenzi mema kujitokeza kwa wingi kushiriki katika harambee hiyo itakayofanyika katika viwanja vya Leaders club,siku ya Jumamosi Julai 4,2015 wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam.kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene.Kulia ni wajumbe wa Kamati hiyo Bi. Mwanamkasi Jumbe na Angela Msangi.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene akiwahamasisha waandishi wa habari kuimarisha mshikamano katika Harambee ya kuwachangia waandishi wa habari wanaosumbuliwa na magonjwa sugu ikiwemo kansa.Kushoto ni Mjumbe wa Kamati hiyo Bi. Grace Nakson.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Zamaradi Kawawa ambaye ni mjumbe wa kamati ya kuratibu Harambee ya kuwachangia wanahabari wanasumbuliwa na magonjwa sugu ikiwemo kansa akiwahamasisha wanahabari wote nchini kuungana katika harambee hiyo kwa kuihamasisha jamaii kushiriki katika tukio hilo muhimu. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya kuratibu Harambee ya kuwachangia waandishi wa habari wanaougua maradhi mbalimbali ikiwemo ugonjwa sugu wa saratani Bw. Benjamin Thompson.
Baadhi ya waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa kuhamasisha kuwachangia waandishi wa habari wanaougua maradhi mbalimbali ikiwemo ugonjwa sugu wa saratani.
Mjumbe wa Kamati ya Kamati ya Maandalizi ya kuratibu Harambee ya kuwachangia waandishi wa habari wanaougua maradhi mbalimbali ikiwemo ugonjwa sugu wa saratani Bi. Angela Msangi akiwahamasisha wanahabari kujitokeza kwa wingi katika harambee hiyo na pia kutumia taaluma yao kuihamasisha jamii kujitolea katika kufanikisha lengo la harambee hiyo. Kushoto ni Mjumbe wa Kamati hiyo Bi. Mwanamkasi Jumbe. PICHA NA FRANK MVUNGI-MAELEZO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...