Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu wa Maafa imeandaa mafunzo ya kujikinga na maafa kwa watumishi wa umma ili wapate uelewa wa mbinu za kujiandaa na kukabiliana na maafa hususan katika sehemu zao za kazi.
Akiongea wakati wa Ufunguzi wa mafunzo ya menejimenti ya maafa mjini Dodoma leo.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu aliyewakilishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Shughuli za Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu, Obbey Assery, alieleza kuwa wameanza kutoa mafunzo hayo kwa watumishi wa ofisi ya Waziri Mkuu na watumishi wengine watajengewa uwezo wa Menejimenti ya maafa.
“Tumeanza na ofisi yetu na baadae watumishi wengine watapata mafunzo haya ili tuweze kuwajengea uelewa na ujuzi wa kukabili maafa husususan katika sehemu zao za kazi. Kumekuwepo na majanga ambayo huwapata watumishi wa umma wakiwa kazini kama vile; moto, matetemeko na ajali lakini kwa kuwa na uelewa wa menejimenti ya maafa hayo tunaweza kuwa na uwezo wa kukabili na kupunguza athari za maafa hayo” alisema Asserry.
Awali akimkaribisha Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kufungua Maonesho hayo, Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig. Jen, Msuya amesema kuwa pamoja na kuwajengea uwezo wa menejimenti ya maafa watumishi hao, alibainisha kuwa kila mshiriki hana budi kuifikisha elimu hiyo aliyoipata kwa jamii inayomzunguka.
Washiriki wa mafunzo hayo wanafundishwa kuhusu ; Dhana ya Menejimenti ya Maafa Mfumo wa Menejimenti ya Maafa Nchini, Huduma ya Kwanza kwa Jamii Uratibu na Udhibiti wa eneo la Maafa na Kujianda na Kukabiliana na dharura ya Moto.
Mafunzo hayo yameendeshwa na Idara ya Menejementi ya Maafa ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na wawezeshaji wengine kutoka Jeshi la Polisi, Jeshi la Zima Moto na Uokoaji pamoja na Taasisi ya Ultimate Security Ltd, kwa ufadhili wa Shirika la Mpango wa Maendeleo Duniani (UNDP) kupitia miradi inayoratibiwa na Ofisi hiyo ya Menejimenti ya Maafa na Mfumo wa taarifa za tahadhari za mapema nchini.
Mkurugenzi Idara ya Uratibu Shughuli za Serikali, Ofisi ya Waziri Mkuu, Obey Assery akisiitiza jambo wakati akifungua mafunzo ya menejimenti ya maafa kwa watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Mjini Dodoma leo.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Uratibu Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Naima Mrisho akisisitiza jambo wakati akitoa mafunzo ya menejimenti ya maafa kwa watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Mjini Dodoma
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...