Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ametoa wito wa kutunza mali asili na mazingira kwa sababu ni urithi kwa vizazi vijavyo. 
Aliongea hayo alipokuwa akifungua mkutano wa Wadau unaohusiana na Azimio la Gaborone jijini Dar es Salaam. 
Aliongeza kuwa idadi ya watu duniani inazidi kuongezeka hivyo basi ni jukumu la kila mmoja kuacha kukata miti hovyo, kuacha kuchoma misitu na vitu vyote vinavyosababisha uharibifu wa mazingira kwa sababu upo uhusiano wa karibu sana kati ya umaskini na uharibifu wa mazingira. 
'Uharibifu wa mazingira huongoza kusababisha umaskini' alisema Bi Samia. Aidha alisisitiza kuwa matokeo yataonekana iwapo maazimio yaliyopendekezwa katika Azimio la Gaborone yatatiliwa maanani. 
Mkutano huo wa Wadau wa Azimio la Gaborone umeandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na Serikali ya Botswana. 
Wadau mbalimbali wa mambo ya mazingira kutoka Wizara na Taasisi za Serikali wamehudhuria Mkutano huo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akifungua Mkutano wa Wadau unaohusiana na Azimio la Gaborone juu ya utunzaji Mazingira jijini Dar es Salaam.
Mtoa mada katika Mkutano huo Bwana Carlos Manuel Rodriguez akiwasilisha mada yake 
Sehemu ya Wadau wa Mkuatano huo wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofis ya Makamu wa Rais-Muungano, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan(hayupo pichani) wakati akifungua Mkutano huo.
Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi Ofis ya Makamu wa Rais-Muungano, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Wadau waliohudhuria Mkutano huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 25, 2015

    Tusikate miti ovyo, na tuwe na kwaida ya kupanda miti wakati wote ili tutunze mazingira yetu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...