Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh.William Vangimembe Lukuvi akikata utepe kuzindua ujenzi wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC Mjini Kahama. Kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Bw. Felix Maagi
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi(aliyevaa miwani) akiweka jiwe la msingi katika nyumba zilizojengwa na NHC Wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Hizi ni miongoni mwa nyumba 50 za gharama nafuu zilizojengwa na NHC katika mtaa wa Bukondamoyo kata ya Mhungula katika halmashauri ya Mji Kahama mkoani Shinyanga. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi nchini Mh.William Vangimembe Lukuvi ameweka jiwe la msingi katika nyumba hizo.
Kaimu Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki wa NHC Bw. Haikamen Mlekio akitoa maelezo kwa Waziri Lukuvi kuhusu hatua zilizofikiwa katika mradi wa nyumba 50 zinazojengwa na NHC Wilayani Kahama ulioanza kujengwa mwezi Januari mwaka 2015 na kutarajiwa kukamilika mwezi Desemba 2015.
Waziri Lukuvi akitizama michoro ya mradi wa nyumba 50 utakaogharimu kiasi cha shilingi bilioni 2.1 unaotekelezwa na NHC Wilayani Kahama.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi akikagua majengo ya nyumba 50 zinazojengwa na NHC eneo la Bukondamoyo Wilayani Kahama akiambatana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Felix Maagi (kushoto).
NHC na wadau wengine endelea kujenga makazi bora na ya kisasa ya bei ambayo wengi wanaweza kuimudu, kila mtanzania anastahili makazi bora na ya kisasa katika maeneo yaliyopangwa yenye huduma zote
ReplyDelete