Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza Bw. Miraji Mtaturu kushoto wakionyesha magwanda yaliokabidhiwa kwao aiyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wilaya ya Magu,Bi. Juliana Kachilu ambaye amejiunga na Chama cha Mapinduzi kutoka CHADEMA.Zaidi ya wananchama 53 kutoka vyama vya upinzani walijiunga na CCM wakiwemo Chadema 28 na ACT 12 na wengine kutoka vyama vingine.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea magwanda ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la CHADEMA (BAWACHA) Wilayani Magu Bi. Juliana Kachilu ambaye amejiunga na Chama cha Mapinduzi, kushoto ni Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza Bw. Miraji Mtaturu.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha kadi zilizokuwa za wanachama wa chama cha Demokrasia na Maendeleo na vyama vingine mara baada ya wanachama hao kujiunga na CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kituo cha mabasi cha Kisesa wilayani Magu mkoani Mwanza.
Katibu Mkuu huyo amempokea aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la CHADEMA (BAWACHA) Wilayani Magu Bi. Juliana Kachilu ambaye amejiunga na Chama cha Mapinduzi , Kinana yuko katika ziara ya kikazi ya mkoa Mwanza akimalizia mkoa wa mwisho wa Tanzania baada ya kuzunguka mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani akipita katika majimbo yote, wilaya zote hapa nchini na nusu ya Kata na vijiji kwa muda wa miaka miwili akikagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010-2015.
Kinana amesikiliza kero mbalimbali za wananchi na kuzipatia ufumbuzi huku akihimiza uhai wa CCM ambapo pia katika ziara hiyo amekuwa akiongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Nape Nnauye .
Baadhi ya Kadi za wafuasi wa vyama mbalimbali walizoamua kuachia ngazi na kuhamia chama CCM.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akiwahutubia wakazi wa mji wa Kisesa mapema jioni ya leo alipokuwa akimaliza ziara yake ndani ya jimbo la Magu.
Mkuu
wa mkoa wa Mwanza Ndugu Magesa Mulongo akizungumza na wananchi kuhusu
kuiagiza mamlaka ya Mapato TRA na kikosi cha Usalama Barabarani kuenda
katika wilaya kwa ajili ya kutoa huduma za utoaji wa leseni za
uendeshaji vyombo vya moto na kukusanya kodi mbalimbali za vyombo vya
moto ili kupunguza urasimu wa huduma hiyo ambazo zimekuwa zikipatikana
kwenye miji mikuu ya mikoa peke yake.
PICHA NA MICHUZI JR-MAGU-MWANZA
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akiwahutubia wakazi wa mji wa Kisesa mapema jioni ya leo alipokuwa akimaliza ziara yake ndani ya jimbo la Magu.
PICHA NA MICHUZI JR-MAGU-MWANZA
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
Kinana c angegombea uPrezdaa
ReplyDelete