Msafara
wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ukivuka mto kuelekea
katika kijiji cha Ilyanchele wilayani Bukombe wakati akiwa katika ziara
ya kikazi katika wilaya hiyo kuelekea katika kijiji hicho hata hivyo
msafara huo haukuweza kuvuka mto mkubwa wa Ilyanchele na magari
kutokana na kutokuwepo kwa daraja linalounganisha kijiji hicho ambapo
leo ndiyo limewekwa jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo
na Ndugu Abdulrahman Kinana.
Baada
ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa daraja hilo Kinana pamoja na
msafara wake walivuka mto huo kwenye daraja la miti lililotengenezwa kwa
nguvu za wananchi. kisha alipanda pikipiki na kuelekea katika mkutano
mdogo na wananchi wa kijiji cha Ilyamchele ambacho kimo katika msitu wa
akiba kata ya Nyamonge wilayani Bukombe mkoani Geita.
Kinana
yuko katika ziara ya kikazi katika mikoa ya Kagera, Geita na Mwanza
ambapo baada ya kumaliza ziara yake mkoani Kagera sasa anaendelea na
ziara hiyo katika mkoa wa Geita kabla ya kumalizia ziara yake mkoani
Mwanza akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akivuka na wananchi katika daraja hilo.
Wananchi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana alipokuwa akiwahutubia mjini Bukombe,mkoani Geita
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akiwahutubi Wananchi katika mkutano wa hadhara mjini, Bukombe wakati wa ziara yake mkoani Geita
Hili daraja linahitaji kuboreshwa kuwa la kisasa zaidi.
ReplyDelete