Ofisa uhusiano na Matukio wa Airtel, Bi Dangio Kaniki akionyesha
kifaa cha HOME Wi-Fi wakati wa kutangaza ofa kabambe ya Sabasaba
itakayo wawezesha watanzania kupata kifaa cha bure cha ziada pindi
watapokinunua katika viwanja vya maonyesho ya Sabasaba. Pichani, Afisa
Masoko wa Airtel ,Ndevonaeli Eliakimu.
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetangaza ofa kabambe
katika viwanja vya Sabasaba itakayomwezesha mteja kununua kifaa cha
HOME Wi-Fi, chenye uwezo wa kuunganisha zaidi ya vifaa 32 kupata
huduma ya internet kwa kutumia kifurushi kimoja kwa gharama nafuu
zaidi na kuunganishwa kwenye kifurushi cha internet cha 40GB Bure.
Ofa hiyo itamwezesha mteja kununua HOME Wi-Fi, kwa shilingi 195,000/-
na kujipatia Home Wi-Fi ya bure pamoja na kifurushi cha internet
cha 40GB cha bure . Ofa hii inapatikana kwenye banda la Airtel katika
viwanja vya maonyesho ya Sabasaba kwa muda wa kipindi hiki cha
maonyesho.
Akiongea wakati wa kutangaza ofa hii Ofisa uhusiano na Matukio wa
Airtel Bi Dangio Kaniki alisema " Tumeona ni vyema kuwazawadia wateja
wetu kwa kuwapatia ofa hii ya kifaa kitakachowawezesha kuunganishwa
kwenye huduma ya internet kwani mahitaji ya huduma ya internet
yanazidi kuongezeka kwa kasi. Airtel HOME WiFi inaweza kuunganisha
vifaa zaidi ya 32 kwenye huduma ya intenet ya kasi bila kuhitaji
simcard yoyote ya ziada".
"Sambamba na hilo, Airtel HOME Wi-Fi vilevile itaunganisha hadi simu
4 za mkononi zilizoko kokote nchini kwenye akaunti moja na kuwapatia
internet ya kasi ya 3.75G. Kwa sasa wanafamilia na watumiaji wa
intenet Tanzania hawana haja ya kununua vifurushi vya intaneti kwa
kila simu , kompyuta, Television au vifaa vyovyote vinavyoweza
kuunganishwa na internet na badala yake watakachotakiwa kufanya ni
kununua kifurushi kwenye kifaa hiki cha HOME Wi-Fi na kuwawezesha
wote waliounganishwa na kifaa hicho kupata huduma ya intaneti popote
walipo Tanzania na watatumia kifurushi kimoja walichonunua"
"Natoa wito kwa wateja wetu na watanzania kutembelea Banda letu na
kujipatia Home Wi-Fi na kuungalisha kweny internet wakati wote".
Aliongeza Kaniki
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...