Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Ernest Mangu akizungumza na waandishi wa habari leo katika kituo cha Stakishari Ukonga jijini Dar es Salaam, kutokana na Askari wa Jeshi la Polisi  na raia wa eneo hilo kuuwawa na majambazi waliovamia katika kituo hicho usiku wa kuamkia leo. 
Viongozi wa Jeshi la Polisi nchini wakiongozwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Ernest Mangu, wakitembelea maeneo mbalimbali ambayo majambazi walidhuru, katika kituo cha Stakishari Ukonga jijini Dar es Salaam leo.

Na Bakari Issa
ASKARI wa nne wa Jeshi la Polisi na raia watatu wamefariki dunia  katika tukio la ujambazi lililotokea katika kituo cha Polisi cha Stakishari kilichopo Ukonga jijini Dar es Salaam.

Katika tukio hilo watu wapatao nane wamesadikika kuingia katika kituo hicho cha Polisi eneo la Stakishari majira ya saa 4 usiku wa kuamkia leo.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Ernest Mangu amesema lengo la la watu hao ni kutaka kuiba silaha zilizokuwa katika kituo hicho cha Stakishari.

Aidha, amesema wananchi wanapaswa kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa zinazohusu uharifu kwa Jeshi la Polisi.

Pia, kuhusu uvamizi wa Majambazi, Mangu amesema watajitahidi kuanza kuimarisha ulinzi kwa upande wao hususani katika vituo vya Polisi ndiyo baadae kwenda kuimarisha usalama wa  wananchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 14, 2015

    Kama kituo hiki hakijajengewa uzio kijengewe na kuwa na lango moja, tunakoelekea ulinzi wa alarm na buttons na back up cars unatakiwa katika vituo vyote vya polisi tukianzia kwanza na vile vilivyoko jijini Dar. Polisi zertu ziwe na vifaa vya command and control vya digital vya kisasa kabisa. Hili tukio lisipite tu hivi bila kuinua vitendea kazi vya polisi na wapatia fungu la dharura kwa ajili ya vifaa vya kisasa. Ulinzi uimarishwe kabisa vibaka wasi pate mahali pa kuchezea.

    Waliopoteza maisha ni watoto wa watu. Poleni wafiwa mliopoteza askari na raia waliokuwa wamekuja kuhudumiwa polisi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...