Na Mwandishi Maalum, New York.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, amezitaka pande zinazopingana nchini Burundi kubaki watulivu na kurejea mara moja katika meza ya majadiliano jumuishi ya kisiasa ili kumaliza tofauti zao na kujadili changamoto zinazolikabili taifa lao.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Katibu Mkuu, Julai 23, Ban Ki Moon ametambua hali ya Amani na utulivu iliyotawala wakati wa uchaguzi wa Rais wa nchi hiyo ( Burundi )uliofanyika Julai 21 na kuwataka wadau wakuu kurejea katika meza ya majadiliano.

Taarifa hiyo imebainisha kwamba Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, anazikumbusha mamlaka za Burundi wajibu wao wa kuwahakikishia usalama pamoja na kuwalinda raia wake na kumalizwa kwa matukio ya uvunjifu wa Amani na uwajibikaji kwa wa ukiukwaji wa haki za binadamu.

“ Katibu Mkuu anatoa wito kwa wadau wote wa Burundi kushiriki kwa nia njema katika majadiliano ya kisiasa kwa kuweka mbele maslahi ya Burundi kwanza, na kutekeleza kikamilifu vipengele vilivyoainishwa katika tamko la Julai 6 la Mkutano wa Kilele wa Jumuiya ya Afrika Mashariki chini ya usimamizi wa Rais Yoweri Museven wa Uganda” Aidha taarifa hiyo inaeleza kuwa, Umoja wa Mataifa utaendelea kufanya kazi kwa karibu na Jumuiya ya Afrika Mashariki ( EAC) na Umoja wa Afrika ( AU) katika kusaidia upatikanajji wa suluhu ya kudumu nchini Burundi.

Katika muktadha huo, Katibu Mkuu anakaribisha kupelekwa watazamaji wa haki za binadamu kutoka AU na wataalam wa masuala ya kijeshi kwa lengo la kusaidia na kupunguza kujitokeza kwa vitendo vya uvunjifu wa Amani na kuwezesha suluhu la Amani la kisiasa kwa matatizo yanayoiathiri nchi hiyo.
" Nimepiga kura ndivyo anavyoelekea kusema mama huyu Raia wa Burundi mara baada ya kupiga kura ya uchaguzi wa rais uliofanyika Julai 21. ( picha kwa hisani ya Umoja wa Mataifa. Ban Ki Moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ametoa wito kwa pande zinazopingana kurejea katika meza ya mazugumzo mara moja baada ya kuwa uchaguzi huo umefanyika kwa amani ili kujadiliana na kumaliza tofauti zao kwa maslahi ya wananchi wao na nchi yao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...