Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela Kairuki (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Edward Marks wakionyesha mfano wa funguo kuashiria uzinduzi rasmi wa huduma ya mikopo ya nyumba iliyopewa jina ya ‘Hamia Kwako’ ya benki hiyo jijini Dar es Salaam leo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Edward Marks (wa pili kushoto), akibadishana mawazo na Ofisa Fedha Mkuu wa Shirika la Mikopo ya Nyumba la Tanzania Mortgage Refinance (TMRC), Oswald Urassa (wa tatu kushoto) katika hafla ya uzinduzi rasmi wa huduma ya mikopo ya nyumba iliyopewa jina ya ‘Hamia Kwako’ ya Benki ya NBC jijini Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa NBC, Mussa Jallow, Mkuu wa Kitengo cha Mikopo Rejareja cha benki hiyo, Isdory Msaki na Mkuu wa  Rasilimali Watu wa benki hiyo, Flora Mollel Lupembe.
 Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela Kairuki (wa pili kushoto), akibadilisha mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Edward Marks (kulia) na Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Rukia Mtingwa (katikati yao), wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa huduma ya mikopo ya nyumba ya Benki ya NBC jijini Dar es Salaam leo.
 Kaimu Mkurugenzi wa Mikopo ya Makampuni wa Benki ya NBC, Salehe Mohamed (kushoto), akiagana na Ofisa Fedha Mkuu wa Shirika la Mikopo la TMRC, Oswald Urassa baada ya hafla hiyo. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi, Mussa Jallow na Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Edward Marks.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela Kairuki (wa pili kulia), akizungumza na Ofisa Fedha Mkuu wa TMRC, Oswald Urassa (kulia) wakati wa hafla hiyo. Wengine kutoka kushoto ni maofisa mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Joseph Haule na Michael Mbago.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...