
Zahara Muhidin Michuzi akiweka sahihi katika kitabu cha wageni alipowasili katika ofisi za CCM mkoa wa Tabora ili kuchukua form ya kugombea viti maalum kwa vijana.
Binti huyo wa Michuzi mara baada ya kuhitimu elimu yake ya shahada yake ya uchumi UDOM ameona ni vyema akawatumikia wananchi wa nyumbani kwake mkoani Tabora kwa kutangaza nia ya kugombea ubunge wa viti maalum kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi.

Zahara Michuzi (kushoto) na Mwasham Hashim (kulia) karani wa UVCCM Tabora akitoa maelekezo ya uchukuaji wa form hizo.

Zahara Michuzi akikabidhiwa form yake leo katika ofisi za UVCCM mkoa-Tabora

Zahara akiifurahia form yake ya Ubunge wa viti maalum Tabora.

Zahara (kushoto) akilipia fedha ya form hiyo huku mama yake mlezi, Rehema Saidi (katikati), akishuhudia kitendo hicho. Picha na Aloyson Blog wa TBN kanda ya Magharibi.
The mdudu, hongera sana mjomba Michuzi kumbe una kabinti? sasa kama kaamua kugombea wala msijisumbue kupiga kampeni maana huyo ashapita bila ya kupingwa hana mpinzani,,,, ila mm The mdudu nishahama vyama vyote na nimehamia ACT Wazalendo nimevutiwa na AZIMIO LA TABORA + LA ARUSHA na hao kanjibai fisadiz watafute pakukimbilia maana nnausongo nao ile mbaya.
ReplyDeleteHIYO NIMEIPENDA,NITAKUJA KUMPIGIA KAMPENI HUYO.
ReplyDeleteTunakutakia heri njema mama ushinde.
ReplyDeleteKumbe Michuzi wa kukaya? kila la kheri kwa mwanao.
ReplyDeleteHongera Sana Zahara...uongozi upo nafsini mwako,natumai utafanya vyema kama ulivyofanya vyema kwenye uwakilishi kama huo Chuoni!!
ReplyDeleteSALUTE MJOMBA KWA KUKUZA. Lakini dukuduku langu ni hizi siasa za bongo ambazo nitafurahi kama wadau watanisaidia? Nimenotice watu wanakurupuka na kuchagua sehemu za kugombea bila kigezo muhimu cha UKAZI WA LILE ENEO FOR A CERTAIN PERIOD OF TIME. Sifahamu kigezo cha NEC kinataka uwe na hiyo address kwa muda gani kabla haujaitwa mkazi. Miss Tanzania ndio waliokuwa wanaitumia hii style kwa kuwaallocate wasichana wazuri kwenye maeneo mbalimbali just to qualify them kwa final. Kama huu utamaduni unaachwa uingie kwenye siasa, then sisi REALLY wenyeji wa huku songombingo tumeisha. Mungu Mpenzi uturehemu.
ReplyDeleteTwamtakia Binti yetu kila la kheri. Aidha hongereni wote kwa malezi mema.
ReplyDelete