MKURUGENZI wa Msama
Promotions, Alex Msama amewaita Maaskofu
na viongozi wengine wa dini katika uzinduzi wa albamu tatu za mwimbaji nguli
Bonny Mwaitege zinazotarajia kuzinduliwa Agosti 2 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee
jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Msama ambaye
ni mdhamini wa uzinduzi
huo, Maaskofu watafikisha ujumbe wa neno la Mungu kwa karibu zaidi baada ya waimbaji kumaliza
kazi yao jukwaani.
Msama alisema uzinduzi huo unatarajia kusindikizwa na waimbaji
mbalimbali wa Tanzania na nje lengo likiwa ni kufanikisha uzinduzi mahiri wa
albamu hizo. Msama alisema
pamoja na uzinduzi huo kusindikizwa na waimbaji mahiri pia, waimbaji chipukizi
watamsindikiza Mwaitege ambaye hivi sasa anaendelea na mazoezi kuelekea
uzinduzi huo.
Aidha Msama
alisema hivi sasa muimbaji huyo pia anamalizia kurekodi baadhi ya nyimbo
zilizomo kwenye albamu hizo katika majiji ya Mwanza, Arusha, Mbeya na Nairobi. Msama alitumia
fursa hiyo kutoa wito kwa mashabiki wa muziki wa injili kujiandaa na uzinduzi
huo ambao utakuwa ni wa aina yake.
"Maandalizi
makubwa kuelekea uzinduzi wa Mwaitege yameshafanyika, kilicho mbele ni uzinduzi
wa hali ya juu, mashabiki wakae mkao wa kula," alisema Msama na kuongeza. "Uzinduzi
wa Mwaitege utakuwa ni wa aina yake kwa sababu maandalizi yake kwa sababu
yamefanywa kwa ustadi mkubwa, mashabiki watarajie kazi bora zaidi kutoka kwa
muimbaji huyo," alisema.
Bonny Mwaitege
anatamba na nyimbo mbalimbali kama Mama ni Mama, Mke mwema, Wakusamehe, Fungua
Moyo wako, Njoo uombewe na Yesu yupo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...