Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo Bw. Azhar Malik wa Dege eco-Village alisema kwa sasa ujenzi unaendelea na karibu aina ya nyumba apartment 3000 zishakamilika.
Aliongezea kusema kwamba kupitia mradi huu waTanzania watanufaika kwa kupata ajira na pia kuwa na huduma kama hospitali, shule, maduka eneo la Kigamboni.
Mradi huu unajengwa kwenye eneo takriban eka 300 na kampuni hiyo imewekeza zaidi ya dola milioni 350.
Kwa ujumla nyumba aina ya villa ziko 300 na apartment ziko 7400. Mradi huu utakamilika mwaka 2018. Apartment zitakamilika mwaka 2017 na villa mwaka 2018.
Ndani ya mji huu wa Dege Eco-Village wakaazi wake hawatahitaji kwenda popote kwasababu kila kitu kitakuwepo kama shule za watoto, kituo cha polisi, hospitali, supermarket, na kadhalika.
Picha zaidi BOFYA HAPA
Picha zaidi BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...