Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Dk. Willibroad Slaa akiwa kwenye gari katika msafara wa mapokezi kwa ajili ya mkutano wa hadhara wa kuwatambulisha Mbunge wa Kahama, James Lembeli na Mbunge wa Viti Maalumu, Ester Bulaya waliohamia Chadema wakitokea CCM jana jijini Mwanza.
 Msafara ukiendelea kuelekea uwanjani sasa
Mbunge wa Jimbo la Kahama, mkoani Shinyanga, James Lembeli (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Taifa, John Mnyika, wakiwapungia wananchi mikono walipokuwa kwenye msafara wa mapokezi ya Viongozi Wakuu wa Chama hicho wakiwasili jijini Mwanza kwa ajili ya mkutano mkubwa wa hadhara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 22, 2015

    Nowadays ,Michuzi unanifanya niipende blog yako,maaana unaweka hata matukio ya vyama vya upinzani,kuna kipindi nilikuwa nasihi wewe kada wa chama cha kijani..wakati wasomaji sio wa kijani tu

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 22, 2015

    AMECHEMSHA HUYO, MAPOKEZI GANI HAYO WATU 20 TU NDIO AWE RAIS HUYO JAMAA HATA MVUTO HANA,.

    HAO HAO WATU WA ARUSHA NDIO WATAMCHAGUA HUKO KWA KINA LOWASSA

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 23, 2015

    mabodigadi wakakamavu sana hawa.. dah....
    wanamlinda rais ajaye JAMES LEMBELI...hahaaaa

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 23, 2015

    VICHEKESHO VITU!!! NURU IMESHA ANGAZA WAPENDA GIZA WATAENDELEA KUKIMBILIA GIZANI, ACHA AENDE MAANDA NDIE ALIE TAKA KUMSAFISHA FLANI KWA KUTAKA KUMNG'OA PINDA KWA HUJUMA ZISIZO NA MAANA. WATANZANIA WOTE WANAMJUA KUWA NI MTETEZI WA MAFISADI. TZ inataka wenye uchungu na wananchi kutoka moyoni si uchungu wa kinafki kupitia siasa za keleleeeee na uzushi. Mungu ibariki Tz Mungu ibariki Afrika.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 23, 2015

    hahaaaaaaaa, tunahitaji tinga tinga bana, huyo bunduki hana lolote, mie nilikuwa nampenda sana mwanzo, ila tatizo kampeni zao ni za kukashifu wengine, fanye kampeni za kistaarabu, kashfa, kejeli za nini? oneni tingatinga, kimya kimya anachomuomba Mungu kwamba amsaidie, na hatawaangusha watanzania. sasa nyie kejeli kibao, za nini?, watanzania tuna macho na tuna masikio tunaona na tunasikia, acheni matusi, ili tuwasaidie angalu wabunge muwe nao wengi, ila Rais Bora atatoka CHAMA KUBWA. TINGATINGA JOHN POMBE MAGUFURI JOSEPH.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 23, 2015

    NIWAPE SIRI YA KUSHINDA KURA, SIRI YA KUSHINDA NI HII HAPA MTANGULIZENI MUNGU KATIKA KILA JAMBO MNALOTAKA KULIFANYA, NAJUA MNAJUA KISA CHA GOLIATHI NA DAUD, DAUD ALIKUWA KIJANA MDOGO, GOLIATH LILIKUWA JITU KUBWA SANA NA LA KUTISHA, LILIUA WATU MAMIA KWA MAELFU, WATU WALIMWOGOPA SANA GOLIATH, LAKINI DAUDI ALIYEKUWA KIJANA MDOGO SANA TENA HANA THAMANI KWA WATU, ALIENDA KWA KUMTANGULIZA MUNGU WA MBINGUNI NA ALIWEZA KUMUUA GOLIATHI TENA KWA JIWE DOGO NDANI YA KOMBEO, KILA KITU MTANGULIZENI MUNGU, NA SIO UBABE, KEJELI, KASHFA, WATU WENGI WANAMWAMINI MUNGU, WANASOMA ALAMA ZA NYAKATI, IKIWA MATUSI YAKIINGIZWA MADARAKANI, SIKU MOJA HATA WANANCHI WATATUKANWA. USHAURI WA BURE.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 24, 2015

    Mwisho wa siku wananchi wataamua oktoba..mwaka huu tutaona mabadiliko mengi kwenye siasa cha muhimu viongozi wetu wakubali na kuheshimu maamuzi ya watz ili tusiingie kwenye CIVIL WAR..MUNGU IBARIKI TANZANIA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...