Mgombea Urais alieteuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wa Mji wa Bagamoyo (hawapo pichani) alipokuwa akirejea jijini Dar jana jioni akitokea mkoani Dodoma.Dkt Magufuli amejitambulisha vyema kila alikopita na kupokelewa kwa kishindo katika mikoa na vitongoji vyake aliyopita ikiwemo jijini Mwanza,Geita,dodoma,Morogoro,Pwani na jiji la Dar kwa ujumla.
 Wakazzi wa Bagamoyo wakimsikiliza Dkt Magufuli wakati alipokuwa akijitambulisha kwao na kuwashukuru kwa kujitokeza kwa wingi kumpokea,alipokuwa akitoka mkoani Dodoma kurejea jijini Dar jana jioni.
 Baadhi ya Wakazi wa Mji wa Chalinze wakimsikiliza Mteule wa Chama cha Mapinduzi CCM kwa nafasi ya Urais ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Pombe Magufuli aliposimama mjini hapo kuwashukuru na kujitambulisha kwa Wananchi wa Chalinze alipokuwa akirejea jijini Dar jana jioni akitokea mkoani Dodoma.
 Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Chalinze,ambaye anawania tena nafasi ya Ubunge katika jimbo hilo Mh.Ridhiwani Kikwete akiwasalimia Wananchi wa Chalinze na kumkaribisha Mgombea Urais alieteuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli aliposimama mjini hapo kuwashukuru Wananchi wa Chalinze (hawapo pichani) pamoja na kujitambulisha kwao alipokuwa akirejea jijini Dar jana jioni akitokea mkoani Dodoma.
  Baadhi ya Wakazi wa Mji wa Chalinze wakimshangilia kwa mayowe Mteule wa Chama cha Mapinduzi CCM kwa nafasi ya Urais ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Pombe Magufuli aliposimama mjini hapo kuwashukuru na kujitambulisha kwa Wananchi wa Chalinze alipokuwa akirejea jijini Dar jana jioni akitokea mkoani Dodoma.
   Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Chalinze,ambaye anawania tena nafasi ya Ubunge katika jimbo hilo Mh.Ridhiwani Kikwete pamoja na  Mgombea Urais alieteuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli wakifurahia jambo mjini Bagamoyo,aliposimama mjini hapo kujitambulisha na kuwashukuru kwa kujitokeza kwao kwa wingi kumpokea,alipokuwa akirejea jijini Dar jana jioni akitokea mkoani Dodoma.
 Mkazi wa Bagamoyo akifurahia jambo
 Wananchi wakimshangilia Dkt Magufuli (hayupo pichani) alipokuwa akijitambulisha kwao hapo jana mjini Bagamoyo.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...