
Na Andrew Chale.
Shirika la ndege la Fastjet limeendelea kupanua wigo wake kwa kuanzisha ‘rout’ zaidi za safari zake ikiwa ni kuunganisha Afrika kuwa moja.
Kwa mujibu wa Afisa Mahusiano na Masoko wa Fastjet, Lucy Mbogoro anasema kampuni hiyo inatarajia kuizindua rasmi safari zake kwa kwenda, Malawi.
“Julai 27, Fastjet tutazindua rasmi safari ya kutoka Dar es Salaam-Lilongwe Malawi. Hii inakuwa ni ‘rout’ yetu ya tano katika safari zetu za Kimataifa ndani ya Afrika lengo ni kufikia nchi mbalimbali za Afrika.” Anabainisha Lucy Mbogolo.
Hata hivyo anabainisha kuwa, wanaendelea kutoa elimu mbalimbali kwa wateja wao juu ya huduma ya Fastjet Ambayo imeendelea kuwa bora zaidi kila kukicha huku akisisitiza kwa wateja kufanya ‘booking’ mapema pamoja na kuzielewa sheria na taratibu za usafirishaji wa anga.
Awali Fastjet ilianzia na safari za ndani za kusafirisha abiria ‘rout’ za Mwanza – Dar, Kilimanjaro – Dar na Mbeya – Dar sasa hivi wamevuka mipaka zaidi kwa nchi za Afrika zikiwemo, kati ya Dar – Johannesburg, Dar – Lusaka, Dar – Harare,Dar – Entebbe nah ii inayotarajiwa kuzinduliwa wiki ijayo ya Dar-Lilongwe.
Aidha, Lucy Mbogoro alibainisha kuwa Fastjet itaendelea kusaidia kukuza sekta ya sanaa nchini na Bara la Afrika kwa kuwaunganisha wadau wa sekta hiyo ikiwemo wasanii wa filamu, muziki na sanaa kwa ujumla.
Lucy Mbogoro anasema hayo ambaapo kwa mwaka huu ni mwaka wa pili mfululizo wakiendelea kudhamini tamasha la Filamu za nchi za majahazi maalufu kama ZIFF.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...