Kampuni ya bigright promotion inategemea kuandaa pambano la masumbwi litakalopigwa tarehe 6/9/2015 katika ukumbi wa vijana , kinondoni jijini Dar es salaam.
Katibu wa ngumi za kulipwa ambaye ndie mratibu wa mpambano huo Ibrahim Kamwe (Bigright) amesema pambano hilo limeandaliwa kwa ajili ya kuamsha vijana kujituma na kujijengea mazingira ya kupenda kufanya kazi na sio kukaa vijiweni na kujiingiza katika utumiaji wa madawa na ukabaji.
Bigright promotion ikishirikiana FRIENDS OF DEVELOPMENTS (FOD) yaani rafiki wa maendeleo wanaandaa pambano hilo kwa kuwachezesha mabondia toka sehemu tofauti za Tanzania.
Katika mapambano hayo Mbena Rajabu atazipiga na Twalibu Mchanjo katika pambano la ubingwa wa Taifa kilogram 57. ambapo bondia Dula Mbabe atazipiga na Ambukile Chusa, wakati Haidary Raju atapambana na Mtango Salum kutoka Tanga
Mapambano mengine ni ya Yona Miyeyusho ataezipiga na Hemedi hemed, huku George Allen wa Tanga akizipiga na Mwinyi Mzengela wa Dar es salaam ana Mau Champion wa Tanga atazipiga na Epson John wa Morogoro
Bondia Mohamed Alkaida atapambana na Guzo Hassan
Mapambano hayo ni kutimiza lengo la FoD kushirikiana na bigright katika kuandaa mapambano hayo ili kuhakikisha Tanzania inakuwa na mabingwa wengi wa ngumi katika mikoa yote, na kuhakikisha wanamichezo wengine na wasanii wanafanya vizuri katika fani zao.
"Kwa kuwa FOD ina wafuasi kila kona ya Tanzania imelenga kupigana vilivyo kuhakikisha majiji yanakuwa safi, wasanii na wanamichezo wanafika mbali kuwasaidia wasiojiweza mitaani na mahospitalini.
"Kwa ufupi yatakuwa ni mapambano ya aina yake kutokana na hao mabondia wenyewe kuwa na uchu wa ushindi kwani ni mabondia wazuri, wazoefu na wana wapenzi wengi.
Mratibu wa mapambano hayo Ibrahim Kamwe (Bigright)
Ibrahim Kamwe (Bigright) akiwa na mabondia wanawake anaowapromoti
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...