KIKOSI cha timu ya Friends Rangers, kesho asubuhi kinashuka
kwenye Uwanja wa Azam Complex, uliopo Chamazi Dar es
Salaam, kuvaana na timu ya Azam FC, katika mchezo wa
kirafiki.
Ofisa habari wa klabu hiyo Asha Kigundula, alisema kuwa
mchezo huo utafanyika asubuhi kuanzia saa 2, asubuhi.
Kigundula alisema kuwa wameshukuru kupata mechi hiyo
ambayo itaendelea kuiweka timu yao katika mazingira mazuri
kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi daraja la kwanza.
Alisema kuwa kucheza na timu kama Azam ni sehemu nzuri ya
kukipa kikosi chao mazoezi mazuri, kwa sababu Azam ni timu
bora na inawachezaji wenye uwezo mkubwa hapa nchini.
Kigundula alisema tayari kikosi chao kimeshacheza mechi mbili
za kirafiki, dhidi ya Yanga ambapo ilifungwa mabao 3-2,
mchezo uliyofanyika kwenye Uwanja wa Karume, Ilala Dar es
Salaam.
Mechi nyingi ambayo Friends Rangers ilicheza na timu ya
Mwadui, ambapo timu hiyo ya Magomeni Kagera ilishinda
mabao 2-1.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...