
MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA UNAPENDA KUWATANGAZIA WANACHAMA
NA WANUFAIKA WOTE KWAMBA KATIKA KUBORESHA HUDUMA KWA WANACHAMA WAKE, HUDUMA ZA
VIBALI MAALUM VYA MATIBABU ZILIZOKUWA ZINATOLEWA KATIKA OFISI ZA MAKAO MAKUU YA
MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA, ILIYO KURASINI BENDERA TATU HAZITATOLEWA TENA OFISI
HII ISIPOKUWA KWA WAGONJWA WAPYA WANAOHITAJI VIBALI VYA DAWA ZA SARATANI HUDUMA ZA KUSAFISHA FIGO (DIALYSIS) NA DAWA ZA
KUDHIBITI NA KUONGEZA KINGA KWA
WALIOWEKEWA FIGO PANDIKIZI.
KWA WANACHAMA WALIOKWISHA ANZA KUPATA HUDUMA ZA
VIBALI, WATAPATA HUDUMA HIZO KATIKA OFISI ZA NHIF ZA MIKOA NA BAADHI YA HOSPITALI
KAMA IFUATAVYO:-
· DAR ES SALAAM: HOSPITALI YA MUHIMBILI, MOI, OCEAN ROAD,
BESTA, REGENCY NA TMJ, OFISI YA NHIF ILALA (JENGO LA USHIRIKA-GHOROFA NA.15), KINONDONI (JOSAM HOUSE GHOROFA YA. 4)
NA TEMEKE (MKABALA NA HOSPITALI YA TEMEKE).
· KWA MIKOA MINGINE
VITUO VILIVYOWEZESHWA KUTOA HUDUMA HIZI NI KCMC
(MOSHI), ALMC (ARUSHA), HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA – MBEYA. ZOEZI
LINAENDELEA KUWEZESHA VITUO VINGINE NA TAARIFA ZITATOLEWA.
HUDUMA ZINAZAZOTELEWA VIBALI KATIKA VITUO
HIVYO NI:-
CT SCAN, MRI,
HUDUMA ZA KUSAFISHA FIGO (DIALYSIS), DAWA ZA SARATANI, VIFAA SAIDIZI, DAWA ZA
KUDHIBITI NA KUONGEZA KINGA KWA WALIOWEKEWA FIGO PANDIKIZI, MIWANI YA KUSOMEA
NA NYONGA AU GOTI BANDIA.
MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA UNAOMBA RADHI KWA
USUMBUFU WOWOTE UTAKAOJITOKEZA KATIKA KIPINDI HIKI CHA MABADILIKO.
UKISIKIA/KUSOMA TANGAZO HILI TAFADHALI MWARIFU NA
MWENZAKO.
LIMETOLEWA NA
KAIMU MKURUGENZI MKUU -NHIF.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...