Mhe.
Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania, akipata maelezo kutoka kwa Bw.
Machumu Essaba, Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT),
Mahakama jinsi mfumo wa JSDS unavyofanya kazi Mahakamani. Maelezo hayo
yalitolewa pindi Mhe. Jaji Mkuu alipotembelea banda la Mahakama ya Tanzania.
Pembeni ya Mhe. Jaji Mkuu ni Mhe. Shaban Ally Lila, Jaji Kiongozi wa Mahakama
Kuu ya Tanzania.
Mhe.Mohamed
Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania, akipata maelezo kuhusiana na Mahakama ya
Rufani (T) kutoka kwa Mhe. Phocus Bampikya, Naibu Msajili Mwandamizi, Mahakama
ya Rufani (
Mhe.
Jaji Mkuu akipata maelezo kutoka kwa Afisa wa Polisi alipotembelea banda la
Polisi katika ziara yake uwanjani hapo.
1.
Mhe.
Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania (katikati), akiongea na Waandishi
wa Habari (hawapo pichani) alipotembelea Banda la Mahakama ya Tanzania, kushoto
ni Mhe. Shaban Ally Lila, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kulia ni
Bw. Edwin Rutageruka, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara (TANTRADE), katika
mkutano huo na Waandishi wa Habari, Mhe. Jaji Mkuu alieleza juu ya mikakati
mbalimbali ambayo Mahakama inayo yenye lengo la kuboresha huduma ya utoaji haki
nchini na kuwataka wananchi kutembelea banda la Mahakama ili kupata elimu hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...