Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akiwa na Balozi Ramadhan Mwinyi, Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.
Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akiwa na Mkuu wa Utawala, Bi Lilian Munanka, ambaye Balozi amemwelezea kama Afisa Mkuu Mwandamizi, mweledi, mchakapakazi, anayejituma na mwajibikaji, mwenyeuzoefu mkubwa na nguzo ya kutegemewa na ambaye amewapokea Mabalozi wengi.
Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akiwa na baadhi ya maafisa na wafanyakazi wa Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa wakiongonzwa na Balozi Ramadhani Mwinyi.
Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula, amewaaga watanzania waishio nchini Marekani, kwa kuwataka kujivunia utanzania wao na kutoionea aibu lugha yao ya taifa, Kiswahili.
Mwishoni mwa wiki, Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani, uliandaa hafla ya aina yake ya kumpongeza, kumshukuru na kumuaga Balozi Liberata Mulamula ambaye sasa ni Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Hafla hiyo iliyowajumuisha watanzania wa kada mbalimbali wakiwamo maafisa na wafanyakazi wa Uwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, wakiongozwa na Balozi Ramadhan Mwinyi, ilipambazwa kwa nasaha mbalimbali na salamu za kumtakia kheri Balozi Mulamula katika jukumu lake jipya.
Hakuna anaeona aibu kuongea kiswahili kwani ndiyo lugha ya kwanza kwa umaarufu africa nzima.
ReplyDelete