Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Business Connexion,Seronga Wangwe akizungumza katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Hayatt Regence jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi mkuu mtendajiwa Kampuni ya Business Connexion, Issac Mophallene akizungumza katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Hayatt Regence jijini Dar es Salaam leo.
Afisa Uendeshaji Mkuu katika Kampuni la Business Connexion, Jane Canny akizungumza katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Hayatt Regence jijini Dar es Salaam leo.
Mwandishi
wa habari wa gazeti la The African, Jastine Amani akiuliza swali
kuhusiana na utendaji kazi wa mitandao ya simu hapa nchini katika
mkutano uliofanyika katika hoteli ya Hayatt Regence jijini Dar es Salaam leo.Kushoto ni mwandishi wa habari wa gazeti la The Gurdian, Frenk Amani.
mkutano uliofanyika katika hoteli ya Hayatt Regence jijini Dar es Salaam leo.Kushoto ni mwandishi wa habari wa gazeti la The Gurdian, Frenk Amani.
MUDA UMEFIKA WA KUPANUA BIASHARA TANZANIA
TANZANIA ina
fursa nyingi ambazo bado hazijatumika. Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, uchumi
unategemewa kukua kwa wastani wa asilimia7.2 mwaka huu na uwekezaji wa serikali
kwa kiasi kikubwa katika mkongo wa taifa unaongeza biashara na upatikanaji wa
teknolojia kwa raia ili kujenga fursa za kusonga mbele kwenye teknolojia zetu.
Pamoja na kuibuka kwa teknolojia nyingi zisizokuwa na mpangilio, hatua hii
imewekwa kwa ajili ya kuongezeka kwa fursa nyingi. Haya ni maoni ya Jane Canny,
Afisa Uendeshaji Mkuu katika Kampuni la Business Connexion.
Kampuni ya
business Connexion Tanzania imekuwa ikifanya kazi tangu mwaka 2000, lengo lake
kubwa hasa ni kujikita katika huduma za kifedha, mawasiliano ya simu, nishati
na madini na sekta ya umma. Kupitia matumizi bunifu ya teknolojia na
ushirikiano wetu na UmojaSwitch Consortium, Tunatoa huduma ya upatikanaji wa
miundombinu ya malipo iliyo salama katika benki 28 na mashine za ATM 200 nchini
Tanzania. Miundombinu hii imeunganishwa na swichi tano za malipo ndani ya
Afrika Mashariki ili kuruhusu miamala ya kimataifa, makampuni makubwa matatu ya
mitandao ya simu ili kuwezesha malipo ya simu na taasisi mbalimbali za serikali
katika kuwezesha makusanyo ya malipo ya kielektroniki.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...