Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es salaam imetiliana saini mkataba wa mashirikiano ya kusaidiana na jiji la Hamburg la Ujerumani. Mkataba huo umesainiwa leo na Mstahiki Meya wa Kinondoni Mhe. Yusuf Mwenda na State Secretary wa Hamburg, Bw. Wolfgang Schmidt, ambapo kutajengwa mtambo wa kisasa wa kuchakata taka za ugani na kuzalishwa mbolea eneo la Mabwepande wenye thamani ya shilingi za kitanzania ni bilioni 3.5 ambazo zitatolewa na jiji la Hamburg.
Mstahiki Meya alisema ukishajengwa mtambo huu sio tu Kinondoni itakuwa safi bali pia ajira 1000 zitatengenezwa na pia mbolea nyingi itapatikana na itatumika kwa faida ya kilimo.
Mstahiki Meya wa Kinondoni Mhe. Yusuf Mwenda na State Secretary wa Hamburg, Bw. Wolfgang Schmidt, wakipeana mikono baada ya kusaini mkataba wa mashirikiano ya kusaidiana na jiji la Hamburg la Ujerumani. Kulia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Eng.Mussa Natty.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...