Kiongozi wa Kundi la TMK wanaume na Mkurugenzi wa kituo cha Mkubwa na Wanawe kinachosimamia bendi ya vijana machachari wa Yamoto, Saidi Fella leo amechukua fomu ya kuomba kugombea udiwani katika kata yake ya Kilungule, wilayani Temeke, jijini Dar es salam.
Saidi Fella ameamua kuchukua fomu hiyo na kugombea nafasi hiyo ili aweze kutatua kero za wakazi wa kata ya Kilungule na kuleta maendeleo katika Kata hiyo.
"Nimeamua kuchukua nafasi hii ili kutatua kero za kata yangu, hapa kuna shida ya maji na barara naamini nikiwa Diwana nitaweza kuonana na wakubwa wa nchi uso kwa uso.
![]() | ||||
Katibu wa Siasa na Uenezi kata ya Kilungule, Juma Ally Kilindo Akimkabidhi fomu ya Kuomba kugombea udiwani Saidi Fella.
|
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...