MODEST SABINUS KWEKA.
14-04-1968 - 25-07-1999
Ni miaka 16 leo,tokea ulipotuacha gafla baada ya kuitwa a Mungu Baba wa Mbinguni.Hatuna cha kusema ila ni kushukuru kwa kila jambo.
Mdogo wetu Modest, tokea hapo maisha ya Familia yetu hayajawa tena mazuri machache Mungu alitukumbuka lakini kubwa kuliko yote, ni kuwa tulimpoteza mama yetu mpenzi mwaka jana, mwezi kama huu, tunaamini upo pamoja naye huko juu nyumbani kwa Bwana.Unakumbukwa sana na Mkeo Mpenzi Constancia, Mwanao wa pekee Kelvin,Shangazi yako Sr. Devotha Kweka, Ndugu zako
Jane, Festo, Eugenia, Elizabeth, Cecilia, na Thadei;Mashemeji zako wote, WaKweka wote wa Narumu, Wamallya wa Manushi, Wafanyakazi wenzako wa Temeke Hospital, wakazi wote wa Temeke Mikoroshini,Ndugu,Jamaa na Marafiki na wote waliokufahamu
Misa ya Kumbukumbu Itasomwa mwanza leo Kanisa la Mt. Augustino – Mkolani Mwanza na Burka – Arusha.
“ RAHA YA MILELE UMPE Ee BWANA”
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...