Je
umekwishawahi kukwama kwenye foleni ukajutia kutobeba gazeti walau likusaidie
kusogeza muda mbele? Je umekwisha wahi kutafuta chanzo cha habari za uhakika
kwenye simu yako ukakikosa?
Je
umekwishawahi kuambiwa kuna tangazo la kazi au tenda ila ukashindwa kuliona kwa
vile lipo kwenye gazeti la siku za nyuma?
Je
umeshawahi kulazimika kuchoma au kutupa magazeti ya siku za nyuma kwa sababu
yamejaa sana nyumbani kwako? Au je umeshawahi kuhisi kuna umuhimu wa kuona
watoto wako wanachojifunza shuleni?
Je
umekwishaona maktaba inayokupa magazeti, majarida au vitabu vyote toka
tulipopata uhuru, mahali popote wakati wowote ulipo?
Kabla hatujaendelea, tazam video hii
ya sekunde thelathini tu https://www.youtube.com/watch?v=x00FXMqY-jg
M-Paper ni
programu ya simu za mkononi, inayokuletea magazeti, majarida na vitabu vyote
kwenye simu yako ya mkononi. Programu hii ya kipekee itakufanya usome
gazeti, jarida au kitabu chote kama kilivyo kwenye makaratasi na si vichwa vya
habari pekee.
Kama
hiyo haitoshi, watengenezeji wa programu hii watakupa shilingi 10,000 pale
utakapodownload app hii ambayo utaitumia kununua magazeti, vitabu na majarida
kabla hujaanza kutumia pesa zako.
Oh,
jambo jingine la kipekee kuhusu program hii ni kuwa, magazeti, majarida na
vitabu vyote vinauzwa kwa nusu bei. Faida mara mbili.
Unaweza
kudownload app hii hapa http://www.mpaper.co.tz
kisha ukaniandikia maoni yako hapa chini, umeionaje? Kumbuka unadownload BURE,
unawekewa 10,000 kwenye akaunti yako hivyo huna cha kupoteza.
Safi sana Mzee,
ReplyDeleteHii itatufaa sana sisi watu wa ughaibuni, maana tunapitwa na habari + matangazo ya magezitini kama tender na vinginevyo.
Hongereni wakuu