Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Dar es Salaam kwenye viwanja vya Zakheem Mbagala kwenye mkutano wake wa kujitambulisha kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam ambapo aliahidi kuwatumikia wananchi na kutenda haki.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wakazi wa jiji la Dar es Salaam kabla ya kumkaribisha mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli kujitambulisha na kuwasalimia wakazi wa Dar es Salaam.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye akiwatambulisha viongozi mbali mbali waliomsindikiza mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli kwenye viwanja vya mikutano vya Mbagala Zakheem.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akipiga ngoma za tumba pamoja na Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye kwenye jukwaa la bendi ya TOT mara baada ya kumaliza kujitambulisha na kuhutubia  wakazi wa jiji la Dar es Salaam.
Waandishi wa habari wakiwa kazini kwenye mkutano wa Dk. John Pombe Magufuli jijini Dar es salaam.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akiwasili kwenye uwanja wa mkutano wa Mbagala Zakheem tayari kwa kujitambulisha kwa wakazi wa Dar es Salaam.
 PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...