Mshindi wa kwanza katika mbio za Kilomita 21, Josepat Joshua (katikati) na wa pili Osward Revelian kutoka Jeshi la Polisi Tanzania wakiimba wimbo wa Taifa baada ya kukabidhiwa medali zao katika uwanja wa Mavuso mjini Mbabane Swaziland katika michezo ya majeshi ya Polisi kwa nchi za Kusini mwa Afrika(SARPCCO) inayoendelea nchini Swaziland.
Mchezaji wa Polisi Tanzania, Mohamed Ibrahim kutoka Jeshi la Polisi Tanzania akirusha tufe katika uwanja wa Mavuso mjini Mbabane Swaziland katika michezo ya majeshi ya Polisi kwa nchi za Kusini mwa Afrika(SARPCCO) inayoendelea nchini Swaziland.Mohamed alichukua nafasi ya tatu katika mchezo wa kisahani na hivyo kufanikiwa kupata medali ya shaba.(Picha na Frank Geofray wa Jeshi la Polisi-Swaziland).
Hongereni sana wawakilishi wetu kwa kutuwakilisha vyema.
ReplyDelete