Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
JAMII imetakiwa kutambua mahitaji ya
watoto wanaoishi katika vituo vya kulelea
katika kubaini changamoto zao
katika maisha wanayoishi na kuweza kuguswa kutoa msaada.
Hayo ameyasema leo Mhasibu Mwandamizi
wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Idara za Serikali na
Mabalozi,Wema Mbaga wakati akitoa msaada wa kituo Khilati Kilichopo Kigogo
jijini Dar es Salaam,amesema kuwa wanatambua umhimu wa kutoa msaada kwa makundi
maalumu wakiwemo watoto wanaolelewa katika vituo.
Amesema kuwa watoto wanachangamoto
nyingi katika ukuaji wao ikichangiwa na kuondokewa na wazazi wao hivyo
wanahitaji faraja kutoka kwa jamii katika kuweza kufikia ndoto zao.
Wema amesema watu wengine wanawajibu
kuwakumbuka watoto katika katika kipindi hiki cha kuelekea Siku Kuu ya Idd
El-Fitri kuwaza kupata mahitaji yao.
Vitu walivyotoa ni Magodoro
,Daftari,Kalamu ,vyenye thamani y ash.milioni 1.5 ambapo ni sehemu ya mchango
wao.
Mkurugenzi wa Kituo hicho ,Khadija
Hussein amesema kutuo kinachangamoto ya
eneo kwani eneo waliopo watoto wanalipia kodi pamoja na matatizo ya chakula.
Amesema watu wenye uwezo watembelee
kituo hicho na kuona mahitaji yao ili waweze kusaidia katika kulea watoto hao
ambao wako 65.
Mkurugenzi wa Kituo cha Watoto
Yatima cha Khayrat,Khadija Hussein akizungumza
na waandishi wa habari juu ya msaada walioupata katika hafla iliyofanyika kituo
hicho ,jijini Dar es Salaam.
Mhasibu Mwandamizi wa Mfuko wa
Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Idara za Serikali na Mabalozi,Wema
Mmbaga akizungumza na waandishi wa habari juu ya msaada walioutoa katika kituo
cha kulele watoto yatima cha Khayrat, katika hafla iliyofanyika kituo hicho
,jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya watoto katika kituo cha
Khayrat wakiwa na daftari zilizotolewa na NSSF Mkoa wa Idara za Serikali na
Mabalozi katika hafla iliyofanyika kituo hicho ,jijini Dar es Salaam.
(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii)
(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...