Na Pius Yalula-MAELEZO
Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa mkutano wa 12 wa watumishi wa umma wa nchi za Afrika ambazo ni wanachama Jumuiya ya Madola utakaonza Jumatatu ijayo jijini Dar es salaam. 
 Mkutano huo unatarajiwa kufunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimimwa  Jakaya Mrisho Kikwete na kufungwa na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma leo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dar es salaam. 
 Amesema kuwa Mkutano huo unatarajia utakaonza tarehe 13 na kumalizika tarehe 15 unatarajiwa kujumuisha nchi 18 za Afrika ambazo ni wanachama wa Jumuiya ya Madola . Bwana Mkwizu amezitaja nchi hizo ni Botswana,Namibia,Cameroon,Ghana,Kenya,Lesotho,Malawi,Mauritius,Msumbiji,Namibia,Nigeria,Rwanda,Sychelles,Sierra Leone, Afrika Kusini,Swaziland,Tanzania,Uganda,Uganda na Zambia. 
Ameongeza kuwa wakati wa mkutano huo washiriki watapata fursa ya kujadili changamoto mbalimbali zinazoukabili utumishi wa umma wa nchi husika na kubadilishana uzoefu ili kuimarisha utendaji na ufanisi katika utumishi wa umma. 
 Aidha Kaimu Katibu Mkuu huyo amesema kuwa wageni hao watapata fursa ya kutembelea mji wa kihistoria wa Bagamoyo,ili kuwapa fursa ya kujifunza hazina kubwa ya kihistoria katika mji huo. 
 Hivyo ametoa wito kwa wananchi wote kuonyesha moyo wa ukarimu kwa wageni katika kipindi chote cha mkutano ili kuendeleza jina zuri la Tanzania.
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais , Menejimenti ya Umma Bwana Hab Mkwizu (katikati) akizungumza na wanahabari jana (leo) jijini Dar es salaam , juu ya Mkutano wa 12 wa Wakuu wa Utumishi wa Umma wa Nchi za Afrika wanachama wa Jumuiya ya Madola utakaofanyika jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 13 hadi 15 mwezi huu. Mkutano huo unatarajiwa kufunguliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Wengine ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasilano Serikalini Florence Temba (kushoto) Mkurugenzi wa Idara ya Rasilimali watu wa Utumishi Bibi Roxana Kijazi. Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dar es salaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...