Mwandishi
wa Habari za Michezo na mdau wa maendeleo ya wilaya ya Handeni, Kambi Mbwana,
mwenye fulana ya CCM, akikabidhiwa fomu ya kuwania Ubunge, Jimbo la Handeni
Vijijini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Katibu Msaidizi wa CCM
wilayani Handeni, Asha Muya, wilayani Handeni, mkoani Tanga. Kulia kwa Mbwana
ni Jerome Mhando, mmoja wa wadau waliomsindikiza katika tukio la uchukuaji fomu
ya kuwania nafasi ya kuwatumikia wana Handeni. Picha na Mpiga Picha Wetu.
Na
Mwandishi
Wetu,
Handeni
MWANDISHI
wa habari za michezo na mdau wa maendeleo wilayani Handeni, mkoani Tanga,
amejitokeza rasmi katika mbio za kuwania ubunge jimbo la Handeni Vijijini kwa
kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Makabidhiano
hayo ya fomu yalifanyika mbele ya Katibu Msaidizi wa CCM wilayani Handeni, Asha
Muya, ikiwa ni siku chache baada ya milango ya uchukuaji fomu za kuwania nafasi
za Ubunge na udiwani kufunguliwa rasmi.Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu
hiyo, Mbwana alisema kwamba ameamua kujitokeza katika mbio hizo za ubunge ili
afanyie kwa vitendo yale aliyokuwa anayapenda, hususan katika suala zima la
maendeleo, huku wachache wao wakishindwa kuelewa faida ya harakati zake,
zikiwapo zile za kuitangaza Handeni kwa njia mbalimbali.
Alisema
wilaya yao imekuwa na changamoto kadhaa zinazohitaji nguvu za pamoja katika
suala zima la shida ya kubwa ya maji, migogoro ya ardhi, ukosefu wa huduma bora
za kijamii, hivyo kunahitajika jitihada na mipango ya pamoja kufanikishaji
mambo hayo.
“Nilikuwa
kimya kwa siku kadhaa nikiangalia akina nani wapo katika mchakato wa kuhitaji
nafasi ya kuwatumikia wananchi wa Handeni Vijijini na kusikitishwa na watu
wasioishi huku na wasiokuwa na uchungu wala dhamira ya kuwakwamua wananchi
wakijitokeza kwa wingi kuwania nafasi ya ubunge, inaonyesha wapo kwa maslahi
yao zaidi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...