MWENYEKITI wa Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha), Leonce Marto amechukua fomu ya kuwania ubunge katika jimbo la Iringa kupitia chama chake hicho.
Amechukua fomu hiyo siku moja tu baada ya Rais Jakaya Kikwete kulihutubia bunge la 10 la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambalo uhai wake utakoma Agosti 20, mwaka huu.
Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, jimbo la Iringa Mjini limekuwa likiongozwa na Mchungaji Peter Msigwa ambaye pia alichaguliwa kupitia Chadema katika uchaguzi wa 2010.
Kwa kupitia taarifa yake aliyoisambaza kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii jana, Marto alisema; “nawasalimu nyote wenye mapenzi mema na Taifa letu la Tanzania na wapenda mabadiliko na demokrasia za ushindani ndani ya vyama vya siasa kwa minajili ya katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 .”
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...