Jeneza lenye mwili wa marehemu Koplo Gaudin Kakoko, likiwa  nyumbani kwa marehemu, Majohe, Ilala Jijini Dar es Salaam tayari kwa mwili wa marehemu kuagwa na wapendwa wake,Mwili huo ulisafirishwa jana kupelekwa kwao wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera kwa mazishi.Marehemu ni mmoja wa askari wanne waliouawa na majambazi hivi majuzi baada ya kukivamia kituo cha polisi Stakishari, Ukonga, Ilala Jijini Dar es Salaam, Mungu ailaze roho ya marehemu wote mahali pema peponi.
Baadhi ya waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu Majohe, Ilala Jijini Dar es Salaam tayari kuuaga mwili wa marehemu Koplo Kakoko amba0 ulisafirishwa jana kupelekwa kwao Wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Ilala(SACP), Lucas Makondya akizungumza na waombolezaji kabla ya mwili huo kuagwa .

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 15, 2015

    Mola ailaze pema peponi roho ya shujaa wetu Koplo Kakoko na awape subra na nguvu familia yake. Inasikitisha watanzania tusivyothamini mchango wa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...