Sikinde
MAGWIJI wa muziki wa dansi nchini, Msondo Ngoma na Mlimani Park Orchestra ‘Wana Sikinde Ngoma ya Ukae’, wataonyeshakana kazi katika Sikukuu ya Iddi Mosi kwenye viwanja vya TCC Club, Chang’ombe.
Msondo
Mpambano huo ujulikanao kama ‘Nani Mtani Jembe’ umeandaliwa na Keen Arts chini ya udhamini wa Konyagi.
Mratibu wa mchuano huo, Joseph Kapinga ‘Kaps’, amesema pambano hilo litakuwa la kusherekea sikukuu ya Idd el Fitr.
Kapinga alisema kuwa pia pambano hilo litaamua ni bendi gani kali kati ya magwiji hao.
“Ni mchuano ambao pia utaamua ni muumbaji yupi bora kati ya Shabaan Dede wa Msondo Ngoma na Hassan Rehani Bichuka wa Sikinde,” alisema Kapinga.
Mratibu huyo alisema kila bendi itapiga kwenye jukwaa lake kama kawaida ili kuondoa malamiko ya kuhujumiwa.
“Pia kutakuwa na michezo aina mbalimbali ya watoto,” alisema Kapinga.
Alisema mchuano huo utaanza saa nane mchana hadi ‘liamba’.
Wadhamini wengine wa shindano hilo ni Saluti5.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...