Mwenyekiti wa CCM, Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikumbatiana na Dkt. John Pombe Magufuli, mara baada ya kutangazwa kuwa ndiye Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, mchana huu hapa kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Dodoma Convition Centre, Mjini Dodoma. Dkt. Magufuli ameibuka kidedea kwa jumla ya kura 2104, wakati wapinzani wake Amina Salum Ally, akiibuka na kura 253 na Dkt. Asha-Rose Migiro, akipata kura 59. Viongozi wakuu wameenda kwenye kikao hivi sasa cha kujua nani atakuwa Mgombea Mwenza wa Urais. hivyo tutaendelea kuwajuza zaidi, endelea kuwa jirani na Libeneke lako pendwa la Globu ya Jamii.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha Dkt. John Pombe Magufuli kuwa ndie Mgombea Urais wa CCM.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mgombea Mwenza wake, Mh. Samia Suluhu Hassan mara baada ya kumtangaza, kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Dodoma Convetion Centre, Mjini Dodoma mchana huu.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha Mgombea Mwenza wake, Mh. Samia Suluhu Hassan wakati akimtambuliasha kwa wanaCCM na Watanzania.
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mh. Samia Suluhu Hassan akipongezwa na Spika wa Bunge, Mh. Anne Makinda pamoja na viongozi wengine. Kushoto ni Waziri Mkuu, Mh. Mizengo Pinda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 12, 2015

    Hongera mpeperusha bendera wa CCM, rais mtarajiwa Dr.John Magufuli. Hongera CCM kwa mchakato mzuri wa kusisimua. Tunashukuru Mungu na kumrudishia utkufu jinsi mambo yalivyokwenda kwa amani. Ninawatakia ushindi katika uchaguzi wa ngazi zote mwezi Oktoba na kampeni zenye hoja na amani. CCM Oyee.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 12, 2015

    Well done jembe letu

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 12, 2015

    Hongera kwa ushindi huu hu tunawatakia ushindi Oktoba.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 12, 2015

    Pinda tabasamu baba!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 13, 2015

    Nimefurahi sana Dkt. John Pombe Magufuli kuwa mgombea urais kwa sababu hana kashfa, mchapakazi na hana mzaha na mtu katika utendaji wa kazi. CCM wamepatia sana kumchagua yeye.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 13, 2015

    Saafi saana. Dkt Magufuli anafaa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. AnonymousJuly 13, 2015

      Kwa kumchagua magufuri ccm imecheza,lakini wangemchagua membe au lowassa kungekua na mgawanyiko ndani ya ccm.

      Delete
  7. AnonymousJuly 13, 2015

    CCM wamefanya la mbolea kumchagua Magufuli. Ni mtu anayekubalika na wengi kwa uchapakazi wake mzuri.

    ReplyDelete
  8. wangemchagua member au lowassa kungekua na mgawanyiko,lakini Kwa kumchagua magufuri ccm imecheza.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 13, 2015

    If u want to succeed please choose a new fresh cabinet with Mwigulu as PM. Waliopo sasa wamechoka na wameshiba. This is my free advice.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 13, 2015

    SASA UFISADI NA RUSHWA IMEPATA MWAROBAINI WAKE, MAWAZIRI JIANDAENI NA JELA

    ReplyDelete
  11. ukawa angalieni angalieni kwenye ubunge, uwakilishi na udiwani ikulu ishapata mtu tayari

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...