Mabanda ya Benki ya NMB katika maonyesho ya saba saba mwaka huu yametia fora kwa kuwa kivutio kikubwa kwa watu wengi kutembelea na kujipatia huduma mbali mbali ikiwemo huduma ya wateja kujaza fomu maalum za kubadirisha kadi zao za ATM kuwa za MasterCard, kuweka na kutoa fedha kupitia gari maalumu pamoja na huduma za NMB Wakala.
Ndani ya viwanja vya saba saba, banda la NMB lipo mtaa wa Mabalozi mkabala na banda la Sido, pia kuna gari maalumu lenye ATM moja na madisisha mawili ya wahudumu (Tellers) wanaofanya huduma zote za kibenki.
Pia kuna mabanda madogo madogo 10, matano ya NMB Wakala ambapo wateja wanaweza kutoa na kuweka fedha zao na mabanda matano yanayotoa huduma za NMB Chap Chap Instant Account ambapo watu wengi wamekuwa wakifurika kwaajili ya kufungua akaunti za NMB.
Pia huduma za mikopo ya fedha na mikopo ya poikipiki za miguu miwili na miguu mitatu kwaajili ya watanzania wanaotaka kufanya biashara ya usafirishaji wa abiria kupitia vyombo hivyo.
Watanzania wote mnakaribishwa kupata huduma bora na ufafanuzi wa bidhaa mbalimbali zinazotolewa na benki ya NMB.
Mkurugenzi wa NMB – Ineke Bussemaker akipata maelezo mafupi kutoa kwa Meneja Masoko wa NMB nje ya banda la NMB lililopo kwenye viwanja vya saba saba leo. Bi Ineke alitembelea maonyesho ya saba saba kwa mara ya kwanza tangu kuteuliwa kuwa mkurugenzi mkuu wa NMB.
Gari la NMB benki la kisasa kabisa kuliko magari yote ya namna hii katika viwanja vya saba saba. Katika gari hili kuna huduma zote za kibenki kama tawi na NMB linalotembea na huduma za ATM ndani yake.
Wateja wakisaini mikataba baada ya kutimiza mashart ya kukopa pikipiki za miguu miwili aina ya Bajaj.
Wateja wakipata huduma za kibenki katika viwanja vya saba saba. NMB Karibu yako.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...