Mapema wiki iliyopita Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilitembelea miradi ya maendeleo katika maeneo mbalimbali nchini ili kukagua utekelezaji wake. Miradi hiyo ni pamoja na Kituo cha kuzalisha samaki Morogoro, Skimu ya Umwagiliaji Iringa vijijini, Maghala ya COWABAMA Iringa Vijijini, Ujenzi wa Barabara ya Iringa – Dodoma, Bwawa la Mtera, Ujenzi wa Barabara ya Manyoni – Itigi, utandikaji wa Reli eneo kati ya Kitaraka na Malongwe, Shamba la Kitengule, One Stop Border Post Mutukula, Mkongo wa Taifa Mutukula na Upanuzi wa mradi wa maji safi, Bomba Kuu la Ziwa Victoria.  

Katika kufanikisha uratibu wa miradi ya maendeleo, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango hufanya ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa miradi hiyo kwa kuzielekeza Wizara zinazotekeleza miradi kuwasilisha taarifa za utekelezaji kila robo mwaka. Aidha, Tume ya Mipango hutembelea miradi ya maendeleo kuona hali halisi ya utekelezaji ikiwa ni pamoja na kubaini mafanikio na changamoto na hatimaye kutoa ushauri katika ngazi husika kuhusu namna ya kukabiliana na changamoto hizo.

Moja ya Majukumu ya Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ni kuratibu utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya Kitaifa ya Kimkakati, Miradi ya Matokeo Makubwa Sasa (MMS) na miradi mingine muhimu kwa ukuaji wa uchumi wa Taifa. Miradi imeainishwa katika Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2011/12 – 2015/16) na ile ya Matokeo Makubwa Sasa iliyoibuliwa katika mfumo wa kimaabara.
Naibu Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango Bibi. Florence Mwanri (wa nne kulia), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mipango na Ufuatiliaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango Bw. Omari Abdallah (wa kwanza kushoto) na maafisa kutoka kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango pamoja na wataalam wa Mradi wa Kituo cha Kuzalisha Samaki kilichopo Kingolwira Mkoani Morogoro wakiangalia sehemu maalum ya kukuzia vifaranga vya samaki baada ya kutotoleshwa.
Naibu Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi. Florence Mwanri (wa pili kulia), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mipango na Ufuatiliaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango Bw. Omari Abdallah (wa kwanza kulia) pamoja na maafisa kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakipata maelezo kuhusu mradi wa ujenzi wa barabara ya Iringa – Dodoma, hatua ulipofikia na changamoto zilizopo kutoka kwa Mtaalamu Elekezi wa mradi Bw.Robin de Kock (mwenye kofia).
Naibu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi. Florence Mwanri (wa tatu kulia) akiangalia kazi ya ujenzi wa barabara ya Iringa – Dodoma inavyoendelea wakati alipotembelea mradi huo pamoja na maafisa kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Pamoja nao ni Mtaalamu Elekezi wa mradi Bw.Robin de Kock (mwenye kofia katikati).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...