Kamanda
wa Polisi Mkoa wa
Dodoma,
SACP David Misime
Napenda
kutoa taarifa fupi kuhusu tukio lililotokea tarehe 11/07/2015 majira ya saa
10:00 hrs huko katika Hoteli ya St. Gasper hapa mjini Dodoma, kuwa wananchi
walitoa taarifa majira ya saa nne asubuhi kwamba kuna mtu mmoja mwenye asili ya
Kiasia amekamatwa na wananchi akiwa na fedha nyingi na kuna vurugu kubwa.
Baada
ya kupata taarifa hizo Jeshi la Polisi Mkoani hapa lilifika eneo la tukio ili
kuona kama taarifa hizo ni za kweli.
Askari walithibitisha kuwa
ni kweli walimkuta mtu mmoja mwenye asili ya Kiasia ambaye alijulikana kwa jina
la AMIT KEVALRAMANI mwenye umri wa miaka 31, Mhindi, Mfanyabiashara, Mkazi wa
Dar es Salaam akiwa na fedha kiasi cha Tshs. 722,500,000/=
ambacho alipohojiwa alisema kuwa tarehe 10/07/2015 alifika Dodoma kwa ajili ya
ununuzi wa mazao ya nafaka.
Alipofika Dodoma tarehe 10/07/2015 majira ya
asubuhi alifikia katika Hoteli ya St. Gasper na tarehe 11/07/2015 aliamua
kurudisha fedha benki kutokana na kuona mkusanyiko wa watu wengi wasioeleweka
na wenye viashiria vya vurugu.

Katika tukio hili na
uchunguzi tulioufanya tumebaini kuwa hakuna kosa la jinai lililothibitika licha
ya kukutwa na kiasi hicho cha fedha, tuhuma za rushwa ambazo ndiyo zilikuwa
msingi wa ukamataji wa mtu huyo hazikuthibitika, kwa kuwa hakuna aliyeona
akizigawa fedha hizo wala hakuna aliyedai kushawishiwa au kugawiwa fedha hizo.
Aidha imethibitika fedha
hizo ni mali yake halali na kwa kuwa hakuna ushahidi mwingine uliyo thibitisha
vinginevyo amerejeshewa fedha zake.
mwisho wa mazingaobwe
ReplyDelete