
Waziri
katika Ofisi ya Rais Kazi Maalum, Prof. Mark Mwandosya ametaka wabunge wote wa
bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhudhuria bungeni kesho ambapo Rais Jakaya Mrisho Kikwete atapoingia bungeni kulihutubia na kulivunja bunge.
Prof.
Mwandosya amesema jambo la Rais kulihutubia bunge ni suala muhimu sana hivyo si
vyema mbunge ama kundi fulani la wabunge kuwepo nje ya bunge wakati Rais
atakapokuwa analihutubia bunge.
Kauli
hiyo ya Prof. Mwandosya ameitoa leo Bungeni, ikiwa siku chache tu kupita tangu
Mkuu wa kambi ya Upinzani bungeni ambaye pia ni Mwenyekiti mwenza wa Umoja wa
Katika ya Wananchi (KAWA) Mhe. Freeman Mbowe kusema wabunge wa umoja huo
hawatarejea tena bungeni.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...