Watawa wa kituo cha kulea watoto yatima cha Mburahati wakipokea msaada wa Mbuzi,Mchele na Mafuta uliotolewa na Rais Jakaya Kikwete, kutoka kwa Kamishna Msaidizi wa Ustawi wa Jamii, Beatrice Fungamo katika hafla iliyofanyika leo katika Mahabusu ya Watoto Jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Kituo cha Darul Alqam, Shaban Mohamed akipokea msaada wa Mbuzi,Mchele na Mafuta uliotolewa na Rais Jakaya Kikwete, kutoka kwa Kamishna Msaidizi wa Ustawi wa Jamii, Beatrice Fungamo katika hafla iliyofanyika leo katika Mahabusu ya Watoto Jijini Dar es Salaam.
Kamishina Msaidizi wa Ustawi wa Jamii, Beatrice Fungamo akizungumza na waandishi wa habari juu ya msaada uliotolewa na Rais Jakaya Kikwete. (picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii)
Na Chalila Kibuda ,Globu ya Jamii
RAIS Jakaya Kikwete ametoa mkono wa Edd El-Fitri katitka vituo mbalimbali vya kulea watoto yatima pamoja wazee wasio na uwezo ili waweze kusherehekea sikukuu hiyo ambayo inatarajiwa kufanyika kesho.
Akizungumza na waandishi habari wakati wa kukabidhi zawadi hizo, kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete, Kamishna Msaidizi wa Ustawi wa Jamii wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ,Beatrice Fungamo amesema kuwa kufanya hivyo ni utamaduni uliowekwa na Rais Kikwete kukumbuka makundi maalum katika siku za sikukuu.
Beatrice amesema zawadi hizo zimetolewa katika mikoa ya Dar es Salaam,Arusha,Kilimanjaro ,Mbeya,Morogoro ,Tanga,Pemba pamoja na Unguja. Ambapo zawadi hizo ni kama Mbuzi, Mchele pamoja na mafuta ya kupikia.
Amesema kwa waliopata msaada huo watumie vizuri katika kuwafanya watoto washerekee sikukuu kama watu wengine.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...