JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
BUNGE LA TANZANIA
  
Kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Marehemu Mariam Salum Mfaki kilichotokea jana tarehe 21 Julai 2015 Saa Nne Asubuhi katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma alikokuwa amelazwa kwa matibabu, Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia yake tunapenda kutoa taarifa ya shughuli ya mazishi kama ifuatavyo:

  • Ratiba ya Mazishi itaanza saa Tisa Alasiri kwa Mwili wa Marehemu kuondolewa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kuelekea Nyumbani kwa marehemu - Ipagala Area E, Dodoma na kufuatiwa na Kisomo cha Hitima na Dua Fupi. Baada ya hapo Mwili utapelekwa Msikiti wa Nunge kwa ajili ya Swala ya Alasiri na kumwombea Marehemu. 
  • Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia ya Marehemu tumekamilisha mipango ya mazishi, ambapo mazishi yatafanyika leo siku ya Jumatano tarehe 22 Julai 2015, Saa Kumi na Moja jioni, Shambani kwake Miyuji nje kidogo ya Mji wa Dodoma. 
Aidha, pamoja na taarifa hii ratiba ya shughuli nzima ya mazishi  imeambatanishwa. 

Imetolewa na:
Ofisi ya Bunge,
Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na
Uhusiano wa Kimataifa,
DAR ES SALAAM

22 Julai 2015

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...