Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania –TRL unasikitika  kuwataarifu wananchi na abiria waliokuwa wasafiri na treni ya leo Ijumaa Julai 24, 2015 kutoka Dar es Salaam kwenda bara kuwa safari hiyo imeahirishwa hadi kesho saa 11 jioni. 
Kwa mujibu wa taarifa hiyo sababu za kuahirishwa safari hiyo ni ajali ya treni ya mizigo iliyotokea leo Ijumaa Julai 24, 2015  saa 8:15 alasiri maeneo  ya  Stesheni  za Mazimbu –Mkata mkoani  Morogoro ambapo ilihusisha mabehewa matano ya  treni ya  mizigo iliyokuwa inasafiri kwenda Bara, manne  yaliacha njia na moja kuanguka kabisa.
Tayari Wahandisi wa TRL wako eneo  la ajali kufanya tathmini na kuanza zoezi la uokoaji,  ikiwemo kazi ya kuyanyanyua mabehewa yaliyopata ajali na kisha kukarabati njia ili iwezwe kupitika mapema hapo kesho.
            Uongozi wa TRL inawaomba radhi wananchi na wateja wake wote nchini  kwa usumbufu             utakaojitokeza.
            -Tamati-
            Imetolewa na Afisi ya Uhusiano ya TRL kwa Niaba ya
            Kaimu  Mkurugenzi Mtendaji ,
            Mhandisi  Elias Mshana
            Dar es Salaam,

            Julai 24,  2015.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...