Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linasikitika kutangaza kifo cha Brigedia Jenerali Dismas Stanslaus Msilu (mstaafu) kilichotokea tarehe 19 Julai, 2015 katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo.

Brigedia Jenerali Dismas Stanslaus Msilu (mstaafu) alizaliwa tarehe 24 September 1938 katika kijiji cha Mlolo, Kata ya Tanangozi, Wilaya ya Iringa Vijijini, Mkoani Iringa. Alijiunga na masomo ya Shule ya msingi na Sekondari na kuhitimu mwaka 1959.

Marehemu Brigedia Jenerali Dismas Stanslaus Msilu alijiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania tarehe 01 Julai 1975. Alistaafu utumishi Jeshini tarehe 23 September 1993.

Marehemu Brigedia Dismas Stanslaus Msilu ameacha mke na watoto. Mwili wa marehemu unatarajiwa kuagwa rasmi tarehe 22 Julai 2015 kuanzia saa 1:30 hadi 2:00 asubuhi katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo na mazishi yatafanyika Mkoani Iringa tarehe 23 Julai 2015.

MUNGU AILAZE MAHALI PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU
BRIGEDIA JENERALI DISMAS STANSLAUS MSILU (MSTAAFU)
AMINA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...