Baadhi ya wakulima wanaoleta alizeti kiwandani hapo wakisubiri huduma ya kukamua mafuta kiwandani hapo. Takribani asilimia 80 ya wakulima wanaoleta alizeti kiwandani hapo wanataka kukamua mafuta ambapo kiwanda kinawalipisha gharama ya kukamua lakini wao wanaondoka na mafuta yao. Jumla ya wakulima 500 wanaleta alizeti kiwandani hapo.
Mkurugezi Mkuu wa Kiwanda cha kukamua mafuta cha Singida Fresh Oil Mills Khalid Omary (mwenye kanzu) akimwonesha Naibu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Mha. Happiness Mgalula sindano iliyochambuliwa na mashine ya kuchambua uchafu kwenye alizeti inayoletwa kiwandani hapo. Anayetazama ni Mha. Omari Athumani, Mchambuzi Sera Mkuu, Tume ya Mipango.
Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha kukamua mafuta cha Singida Fresh Oil Mills Khalid Omary akionesha dumu la mafuta yanayozalishwa na kiwanda chake tofauti na yale ambayo ni feki ambapo watu wasio waaminifu wanatumia nembo ya kiwanda hicho.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Angalizo zuri:
ReplyDeleteHizi picha zinatazamwa, globally; wafanyakazi wanatahadharishwa wavae glovu mikononi. Ni sehemu ya mkakati wa kuongeza thamani (value added strategy).