Mkurugezi Mkuu wa Kiwanda cha kukamua mafuta cha Singida Fresh Oil Mills Khalid Omary (mwenye kanzu) akimwonesha Naibu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Mha. Happiness Mgalula sindano iliyochambuliwa na mashine ya kuchambua uchafu kwenye alizeti inayoletwa kiwandani hapo. Anayetazama ni Mha. Omari Athumani, Mchambuzi Sera Mkuu, Tume ya Mipango  
 Baadhi ya wakulima wanaoleta alizeti kiwandani hapo wakisubiri huduma ya kukamua mafuta kiwandani hapo. Takribani asilimia 80 ya wakulima wanaoleta alizeti kiwandani hapo wanataka kukamua mafuta ambapo kiwanda kinawalipisha gharama ya kukamua lakini wao wanaondoka na mafuta yao. Jumla ya wakulima 500 wanaleta alizeti kiwandani hapo
 Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda cha kukamua mafuta cha Singida Fresh Oil Mills Khalid Omary akiwaonesha wajumbe wa timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Tume ya Mipango machine ya kukamua mafuta ya alizeti
 
 Baadhi ya wafanyakazi wa kitengo cha kupakia mafuta kwenye madumu wakiendelea kupakia mafuta ya ujazo wa lita tano kiwandani 
Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha kukamua mafuta cha Singida Fresh Oil Mills Khalid Omary akionesha dumu la mafuta yanayozalishwa na kiwanda chake tofauti na yale ambayo ni feki ambapo watu wasio waaminifu wanatumia nembo ya kiwanda hicho.  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...